Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Barabara Mlima Kitonga Kutanuliwa Kuwa Njia Nne

SERIKALI iko katika hatua za mwisho za kuanza upanuzi wa barabara ya Kitonga mkoani Iringa ambayo sasa itakuwa ya njia nne na yenye taa za barabarani.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametangaza kwamba hatua hiyo ni uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan ili kupunguza foleni na kuboresha usalama wa watumiaji barabara katika njia hiyo inayotumiwa na magari mengi.

Waziri Ulega aliyekuwa katika ziara ya ukaguzi wa eneo la zaidi ya kilomita saba linalopaswa kupanuliwa, alisema barabara hiyo ni ya kimkakati kwa uchumi wa nchi kwa sababu inatumiwa pia na magari yanayokwenda katika nchi zinazotumia bandari ya Dar wa Salaam kubeba mizigo yao.

“Barabara hii sasa itakuwa ya njia nne - mbili za kwenda na mbili za kurudi ambapo sasa ni njia mbili tu zinatumika. Na tutafunga taa kote ili kuhakikisha muda wote barabara inapitika muda wote, “ alisema Ulega.

Akitoa picha ya ongezeko la uhitaji wa upanuzi wa barabara hiyo, Mbunge huyo wa Jimbo la Mkuranga alisema idadi ya magari yanayopita katika Barabara Kuu ya TANZAM imeongezeka kutoka magari 1,700 hadi 3,400 kwa siku, hali inayopelekea barabara hiyo kuzidiwa na wingi wa magari.

“Nimepokea mapendekezo kutoka kwa Meneja wa TANROADS Iringa ya kuhakikisha tunaondoa msongamano wa magari katika mlima Kitonga, na nimeelekeza kwa wataalamu wetu kupanua hii barabara kwa kilometa 7. Kwa sasa hivi barabara ina njia mbili kwa hiyo tutatanua na kuwa njia nne”, amesema Ulega.

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: