Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Familia Nzima Yafariki kwa Moto Mara

Mtumishi wa Wizara ya Maji, Rochi Mkolekuwa (39), mke wake Mariam Msigwa (34) na mtoto wao, Rochi Shaban (4) wote wamefariki dunia, baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto Mtaa wa Nyarusrya, Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akisema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na uchunguzi tayari umeanza.



Kamanda Magere amesema walipata taarifa ya tukio hilo saa 10 usiku wa kuamkia leo Jumatatu Januari 5, 2026 na walipofika katika nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi walikuta imeteketea na watu hao wakiwa ndani. "Inaonekana taarifa ilichelewa kutolewa na tulipofika pale tulikuta tayari wamefariki dunia, mwili wa baba ulikutwa sebuleni na miili ya mama na mtoto ilikutwa chumbani, tumeanza uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine," amesema Magere.

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: