Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, ASP Jumanne Muliro ametoa onyo kwa yeyote atakaetishia usalama ndani ya mkoa huo katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360, Kamanda Muliro amehoji uhalali kisheria wa kampeni ya No Reforms No Elections ya CHADEMA na ile ya Oktoba Tunalinda Kura ya chama cha ACT Wazalendo akisema ni kinyume cha sheria.
Tazama mahojiano yote.