Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kadri uchumi wa Taifa unavyopanda ndivyo atakavyoendelea kuongeza stahiki na mishahara kwa majaji.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo, Januari 13, 2026, alipokuwa akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania.
Amesema kuwa si kwamba Serikali haitaki kuwafanya watu wote wapate mishahara itakayowawezesha kuishi vizuri, bali changamoto iliyopo kwa sasa ni hali ya uchumi wa Taifa. Hata hivyo, Serikali imejitahidi kwa kadri ya rasilimali iliyopo.
Aidha, Dkt. Samia amesema kuwa pale hali ya uchumi itakapokuwa imeruhusu Serikali itaongeza mishahara, lakini kwa sasa ni muhimu kwenda polepole hadi pale hali ya uchumi itakapokuwa sawa.
Chanzo; Wasafi