Viongozi kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wameshikiliwa na Jeshi la Polisi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti, John Heche wameachiwa huru kwa dhamana hii leo Novemba 10, 2025.
Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa, viongozi hao waliokuwa wakishikiliwa vituo mbalimbali vya Polisi nchini wameachia katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar.
Mbali na Heche, wengine walioachiwa huru ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Bara, Amani Golugwa, Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Boniface Jacob au Boni Yai na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.
Chanzo; Global Publishers