Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Said Habibu Tunda kuwa Mtendaji wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) pamoja na Pius Andrew Ng’ingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka (UDART).
Uteuzi huo umefanyika hii leo Octoba 2, 2025 ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Said Tunda ameteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa huku Pius Ng’ingo akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa UDART, Waziri Kindamba ambaye pia uteuzi wake umetenguliwa.
Chanzo: Millard Ayo