Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Rais Atoa Bilioni 2 kwa Online Media na Content Creator

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Tsh. bilioni 2 kwa Vijana waliojiajiri kupitia taaluma na vipaji vyao kwenye Online Media, Content Creators na Vijana wengine ili waweze kuzitumia kama mitaji ya kujikwamua kiuchumi na kutimiza ndoto zao.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema hayo Jijini Dodoma leo January 30,2026 wakati akiongea na Waandishi wa Habari ambapo amesema kwa Vijana ambao wapo tayari kuchangamkia fursa hizo wafike ofisi za Wakuu wa Wilaya kupitia kwa Maafisa Habari wa Wilaya nchi nzima kuanzia leo hadi February 15,2026 ili wakajiandikishe ili mkakati wa kuwapa fedha uanze.

“Fursa hii ni adimu tumempata Rais ambaye amekubali kusafiri na wewe kwenye ndoto yako, umehangaika kwa muda mrefu pekee yako, ukitumia simu yako, ukikosa vibali vya kwenda hata baadhi ya maeneo kufanya shughuli, wengine wakisema unapoteza muda lakini nikuhakikishie Dkt. Samia amenipatia bilioni 2 ili tukupatie utimize ndoto yako” Amesema Waziri Makonda

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: