Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limetoa ufafanuzi kufuatia taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa Godlove Materu (45), mkazi wa Tunduma, hajulikani alipo baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana.
Polisi wamethibitisha kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo na alikamatwa na askari polisi kwa tuhuma za kupanga na kufanya matukio ya jinai katika maeneo mbalimbali ya mji wa Tunduma na viunga vyake.
Kwa sasa, Jeshi la Polisi limebainisha kuwa uchunguzi dhidi ya Materu umekamilika na hatua nyingine za kisheria zinafuata.
Aidha, wametoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa zisizo na uthibitisho zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na badala yake waendelee kuamini vyanzo rasmi vya habari kutoka kwa mamlaka husika.
Chanzo; Itv