Abiria wanaotumia usafiri wa Mwendokasi wameshuka kupitia madirishani katika Kituo cha Magomeni Mwembechai, jijini Dar es Salaam, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kusimamishwa na polisi kwa madai ya kuzidisha abiria kupita kiasi.
Tukio hilo lilitokea leo asubuhi, majira ya 08:25, ambapo abiria hao walikuwa wakitokea Kimara kuelekea katikati ya jiji.
Baadhi ya abiria walikuwa wametokeza vichwa na sehemu za miili yao nje ya madirisha na wengine kukaa juu ya basi hilo huku wakiimba nyimbo mbalimbali, zikiwemo zenye maneno ya malalamiko kama vile "hatumtaki!"
Chanzo cha hali hiyo kinadaiwa kuwa ni changamoto kubwa ya usafiri katika maeneo ya Kimara na Mbezi, ambapo abiria wanasema wamekuwa wakikaa vituoni kwa muda mrefu tangu alfajiri bila kupata magari ya kutosha kuwapeleka mjini.
Chazo: Nipashe