Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa kuhusu vurugu zilizotokea leo asubuhi katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati mashauriano mbalimbali yakiendelea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema vurugu hizo zilihusisha baadhi ya wana chama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao walikuwa wakipinga uamuzi wa mahakama uliokuwa ukisisitiza kesi ya Tundu Lissu.
Muliro amesema vurugu zilianza baada ya ukumbi kuhaj na baadhi ya wafuasi waliokuwa wakipinga uamuzi wa mahakama, na kufanya fujo na kujaribu kuwashambulia askari waliokuwa wakidhibiti usalama.
Askari wa Jeshi la Polisi walijibu haraka na kufanikisha kutuliza hali ya hewa, huku wakisisitiza kuwa vitendo vya kuwachokoza askari havitavumiliwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ambaye amewataka wananchi kuendelea kuwatulivu na kushirikiana na polisi kwa ajili ya usalama na amani.
Chanzo: Global Publishers