Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, limesema linafanya uchunguzi juu ya tukio la kujinyonga kwa mtuhumiwa Michael Lambau (18), akiwa Mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Moshi Kati, alipokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kumpiga baba yake mdogo kwa mabapa ya panga.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa hapo awali Michael alikuwa anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya baba yake mzazi kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni, kisha akatoroka mpaka alipokamatwa baada ya kumshambulia baba yake mdogo.
Chanzo; Itv