Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameahidi kwenda kumlilia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili atoe Tsh. bilioni 1 au bilioni 2 ambazo zitatumika kuwakopesha Vijana waliojiajiri kwenye Online TV ili waweze kuboresha kazi zao ikiwemo kuwa na vifaa vya kisasa.
Makonda amesema hayo leo January 13,2026 Jijini Dodoma wakati akiongea na Watumishi wa Wizara ya Habari kwenye halfa fupi ya kukabidhiwa ofisi na Waziri Palamagamba Kabudi iliyofanyika muda mfupi baada ya Viongozi hao kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makonda amesema “Vijana wengi wa Taifa hili wamejiajiri kwenye habari hasa Online TV, nitaenda kumlilia Dkt. Samia atupatie fedha bilioni 1 hadi bilioni 2 tuwakopeshe Vijana wawe na vifaa vyao wenyewe ili usirekodi kwa kisimu, urekodi kwa camera ya maana una kompyuta yako ili utengeneze content ambayo Dunia itaona na kuiona Tanzania katika uzuri wake”
Chanzo; Millard Ayo