Mtoto Daniel Jeremiah (15) Mkazi wa Kata ya Olorieni, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha ameripotiwa kutoroka nyumbani kwao anapoishi Mama yake na kumuachia ujumbe ya kuwa anakwenda kujitafuta na kwamba anamuonea Mama yake huruma jinsi anavyomuhangaikia.
Ujumbe huo umesomeka “Mama samahani lakini mimi nimeamua kuondoka naona hii ndio njia peke itakayokufanya usihangaike kunitafutia hela mimi ngoja niondoke nikajitafute wewe kaa mwenyewe, sio kwa ubaya Mama ninakuonea huruma unavyonihangaikia mimi, naomba unisamehe kama nimekosea".
Akizungumza na Ayo Tv, Jackline ambaye ni Mama Mzazi wa Daniael amesema wamekuwa wakiishi vizuri na Mtoto wake kama Marafiki na kwamba hajawahi kumsimulia changamoto yoyote ya maisha ambapo amekuwa akimuhudumia kwa kumpatia mahitaji yote ya muhimu kama Mzazi.
Chanzo; Millard Ayo