Mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwani Kikwete, ametajwa miongoni mwa mawaziri wapya katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika uteuzi huo, Ridhiwani Kikwete amepewa jukumu la kuiongoza Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, moja ya wizara muhimu inayohusika na masuala ya ajira za umma, uwajibikaji wa watumishi wa serikali, na uimarishaji wa mifumo ya utawala bora.
Chanzo; Dw