Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uhalali wa Tume, Mahakama Kutoa Uamuzi

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajiwa kutoa uamuzi Machi 6, 2026, mchana, kuhusu uhalali wa Tume ya Kuchunguza Matukio yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Uamuzi huo unatokana na Kesi Na. 30210/2025 inayopinga uteuzi wa wajumbe wa tume hiyo, inayoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu, Othman Chande Othman. Shauri hilo linasikilizwa na Jaji Hussein Salum Mtembwa katika Mahakama Kuu.

Kesi hiyo imefunguliwa na mwanaharakati Rosemary Mwakitwange, kwa kushirikiana na mawakili Deogratias Mahinyila na Edward Heche, wakimshitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wajumbe wanane wa tume hiyo.

Waombaji wanadai kuwa tume haikuundwa kwa mujibu wa sheria, wakitaja kasoro katika muundo wake, madai ya kukosa uhuru na kuundwa kwa nia mbaya. Pia wanahoji sifa za baadhi ya wajumbe na kuiomba mahakama itengue uteuzi huo.

Kwa upande wao, wadaiwa wanasisitiza kuwa tume hiyo iliundwa kwa mujibu wa mamlaka halali ya kisheria na inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Uamuzi wa mahakama unatarajiwa kutoa mwelekeo wa kisheria kuhusu iwapo tume hiyo itaendelea na majukumu yake au la.

 

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: