Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Serikali Yajibu Meli Iliyokamatwa na Dawa za Kulevya El Salvador

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, imesema meli iliyokamatwa nchini El Salvador ilisajiliwa visiwani Zanzibar kupitia wakala.

Msigwa ametoa kauli hiyo leo Februari 26, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua za haraka ikiwemo kufuta usajili wa meli hiyo, kuwatafuta wamiliki wake pamoja na kutoza faini ya dola za Marekani 20,000, licha ya ushirikiano kutoka kwa wahusika kutokuwa wa kuridhisha.

Serikali imeeleza kuwa inaendelea kufuatilia suala hilo kwa karibu.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: