Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema uzinduzi wa Barabara ya Juu (Flyover) ya Mwanakwerekwe, umeandika historia kubwa ya maendeleo ya Zanzibar, hasa katika kipindi ambacho visiwa hivyo vinaadhimisha miaka 62 tangu kufanyika kwa Mapinduzi ya mwaka 1964.
Akizungumza leo Januari 6, 2026, wakati wa uzinduzi rasmi wa barabara hiyo ya juu ambayo ni ya kwanza kujengwa Zanzibar, Dk. Mwinyi amesema maendeleo ya kweli na endelevu yanajengwa kupitia uwekezaji katika miundombinu imara na ya kisasa inayokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.
Amesisitiza kuwa ‘flyover’ hiyo ni kielelezo cha dhamira ya serikali katika kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafiri na uchukuzi, hususan katika maeneo ya mijini yenye msongamano mkubwa wa magari.
Chanzo; Nipashe