Wanafamilia watano wa familia ya Francis Kaggi, wamefariki dunia baada ya kupata ajali, wakitoka kwenye maziko mkoani Tanga.
Taarifa iliyosambazwa miyandaoni huku ikionesha wanafamilia hao, pamoja na ratiba ya mazishi, imewataja walifariki kuwa ni Francis Kaggi, na wanawe waanne Janemary Kaggi, Maria Kaggi, Joshua Kaggi, Elineema Kaggi.
Imeeleza kwamba, Mtoto wake wa pili alitarajia kuanza elimu yake ya juu Chuo Kikuu Ardhi (ARU), na wa kwanza wa kike alikuwa anafanya kazi mkoani Tabora na mdogo alikuwa anasoma shule ya awali. Na mwingine alikuwa anafanya kazi Tanesco.
Chanzo cha vifo ni ajali, wakitoka kumzika mama wa mumewe siku ya Alhamisi, na Jumapili walianza safari asubuhi, huku mume ambaye ni Francis, akiwa ni dereva wa gari hilo.
Inaelezwa mkewe Francis, pekee amenusurika ajalini, na dada wa kazi akiwa amelazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU).
Chanzo; Nipashe