Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanaopita Barabara ya Mwendokasi Waonywa

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza limetoa onyo kali kwa madereva wa magari na pikipiki wanaokaidi sheria kwa kutumia barabara za mabasi ya mwendokasi (BRT), likisisitiza kuwa muda wa kutoa elimu umekwisha na sasa ni wakati wa hatua kali za kisheria.

Akitoa taarifa hiyo leo, Januari 31, 2026, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, SACP Jumanne Muliro, amesema kuwa kumeibuka wimbi la madereva wakaidi ambao wamepoteza lengo la kuwepo kwa usafiri huo wa umma kwa kuingilia njia hizo na kusababisha hatari ya ajali mbaya.

Kamanda Muliro ameeleza kuwa kitendo cha dereva wa mwendokasi kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki au gari dogo lililoingia kwenye njia yake kinaweza kusababisha basi hilo kupata ajali na kuhatarisha maisha ya abiria wengi lililowabeba.

 

 

Chanzo; East Africa Radio

Kuhusiana na mada hii: