Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Shura ya Maimamu Yalaani Yaliyotokea Oktoba 29

Shura ya Maimamu Tanzania imelaani vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyoripotiwa kutokea katika siku ya Uchaguzi Mkuu uliopita Oktoba 29, mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Shura hiyo, Sheikh Issa Ponda, akisema wanasimama na ndugu, jamaa na familia za wahanga, huku wakituma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Sheikh Ponda amedai kwamba katika vituo vingi zoezi la kuhesabu kura halikufanyika ipasavyo, mawakala hawakupewa nakala za majumuisho, na majumuisho ya kata hayakuripotiwa kufanyika katika baadhi ya maeneo.

Aidha, Shura hiyo imelaani kile ilichokiita ufisadi na ulaghai katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

"Shura ya Maimamu inapendekeza viongozi wa dini, viongozi wastaafu na taasisi za haki za binadamu kusaidia kuiunganisha serikali ya CCM na upinzani kwa mazungumzo ya kitaifa. Pia inatoa wito wa kuanza mchakato wa katiba mpya," amesema.

Pia Sheikh Ponda amesema maombi yao ni kwamba Tanzania ibaki na amani, mshikamano na uhuru wa kweli.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: