Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu hadi kesho Februari 19 baada ya Shahidi wa 12 kufiwa na Mkwewe.
Kesi hiyo yenye namba 19605 ya mwaka 2025 ilisikilizwa leo mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Dunstan Nduguru ambapo Shahidi wa 11 wa Jamhuri P7 alitoa ushahidi wake.
Nje ya Mahakama, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amezungumzia mwenendo wa ushahidi katika shauri hilo.
Chanzo; Millard Ayo