Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waganga wa Jadi Waomba Kutambuliwa Kitaifa

aganga wa jadi katika Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora wameeleza kusononeshwa na kitendo cha kutotambulika rasmi kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa, licha ya mchango wao mkubwa katika jamii.

Mwenyekiti wa waganga hao aliwasilisha kilio hicho mbele ya Katibu wa NEC, Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa CCM, Ndg. Kenani Kihongosi, wakati wa ziara ya viongozi hao mkoani Tabora ya kukagua uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi.

Akijibu ombi hilo katika mkutano wa hadhara, Katibu wa Uenezi, Kenani Kihongosi, aliwahakikishia waganga hao kuwa Serikali na Chama Cha Mapinduzi vinatambua na kuthamini umuhimu wao katika utamaduni na ustawi wa jamii.

Katika kuonyesha utambuzi huo kwa vitendo, Kihongosi aliwakaribisha viongozi wa waganga hao kuketi katika meza kuu ya viongozi, hatua iliyopokelewa kwa furaha kama ishara ya heshima na ushirikishwaji wa kundi hilo katika shughuli za kiserikali na kisiasa.

 

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: