Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wachina wa Bilioni 6 Waburuzwa Kortini

Raia wawili (2) wa China ambao ni Weisi Wang (41) na Yao Licong wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha takribani Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Kumi na Tatu za Kitanzania.

Washtakiwa hao wamesomewa makosa yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita na Benjamin Muroto mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa Mahakamani hapo leo Januari 07, 2026 washtakiwa wote wawili (2) wanakabiliwa na kosa la kwanza la kuongoza genge la uhalifu, ikielezwa kwamba walitenda kosa hilo tarehe tofauti kati ya Disemba 01, 2024 na Disemba 30, 2025, katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Unguja -Zanzibar, pamoja na maeneo mengine ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, imeelezwa Mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa makusudi waliandaa genge la uhalifu lililojihusisha na kughushi nyaraka, kunakili kadi za ATM, kukwepa kodi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Katika kosa la pili, washtakiwa wote wanatuhumiwa kutenda utakatishaji fedha, ambapo imeelezwa Mahakamani hapo kwamba katika tarehe hizo hizo za kati ya Disemba 01, 2024 hadi Disemba 30, 2025 wakiwa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washtakiwa walijipatia mali ambazo ni Dola za Kimarekani 707,075 pamoja na Shilingi za Kitanzania 281,710,000, huku wakijua wazi kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu wa kuongoza genge la uhalifu.

Baada ya kusomewa mashtaka, hayo, Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki alisema kuwa washtakiwa hao hawatakiwa kujibu chochote kwa sasa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Pia kwa mujibu wa sheria, mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana hivyo hawawezi kupata dhamana katika ngazi ya Mahakama hiyo.

Upande wa Jamhuri uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa, ambapo kesi imeahirishwa hadi Januari 21, 2026.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: