Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ukosefu wa Kipato Sababu ya Wanawake Kupitia Ukatili wa Kijinsia

Zaidi ya Wanawake 60 waliokumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukatili wa kijinsia, wamepatiwa mafunzo ya urembo bure ikiwa ni hatua ya kuwainua na kuwawezesha kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha urembo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Uongozi (MnU) Shamira Mshangama,  amesema ili kufanikisha hilo wamezindua rasmi saluni iitwayo Mwanamke na Uongozi Saluni, itakayotoa mafunzo ya urembo wa nywele, kucha na vipodozi (make-up) bure kwa muda wa miaka miwili.

“Tunawawezesha wanawake kushiriki katika nafasi za maamuzi na uongozi. Leo tunazindua Mwanamke na Uongozi Saluni. Tangu mwaka 2017 tulipoanza, tuligundua changamoto za ukatili ambazo wasichana wanapitia, na sababu kubwa ni ukosefu wa kipato binafsi. Kwa kushirikiana na mfadhili wetu, Women First International Fund, tumeanzisha mradi huu,” amesema.

Amesema mradi huo unaitwa ‘Nafasi ya Kuanza Upya’, ambapo watatoa mafunzo ya urembo bure kwa lengo la kuwawezesha wanawake kujipatia kipato binafsi. Pia amesema taasisi hiyo itatoa ajira katika ofisi yake, huku walengwa wakuu wakiwa ni wanawake wanaopitia changamoto za kijinsia.

“Tunataka kuhakikisha wasichana wengi wanapata mafunzo. Hiki kitakuwa kituo cha mafunzo kwa wasichana kujifunza urembo. Pia taasisi itajipatia kipato kitakachoiwezesha kuwafikia mabinti wengi zaidi kupitia miradi ya kuwainua kiuchumi,” ameongeza.

 

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: