Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) ameishauri Serikali kupunguza masharti ya Vijana kupata mikopo ili kuwawezesha kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza Bungeni wakati wa kuchangia Mpango Elekezi wa Maendeleo ya Muda Mrefu wa Taifa 2026/27 – 2050/51 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Bajeti ya Serikali kwa kipindi cha 2026/27 – 2028/29, Baba Levo amesema Vijana wengi wana nia ya kujiajiri lakini hukwamishwa na ukosefu wa mitaji jambo linalowafanya washindwe kuanzisha biashara au miradi ya kiuchumi.
“Vijana hawataki konakona wanataka hela naomba mpango huu upunguze konakona kwenye namna ya kumfikishia Kijana hela, Kijana anataka pesa na nitawaambieni ukweli tumekuwa tukisisitiza Vijana kujiajiri Wazee kujiajiri lazima uwe na hela huna hela unajiajirije? biashara naifungua na nini? tupunguze masharti ya Vijana kuweza kukopa” - Clayton Revocatus Chipando, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini.
Chanzo; Millard Ayo