Baada ya uteuzi, kisha kuidhinishwa na bunge, hatimaye Dk Mwigulu Nchemba ameapishwa rasmi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Mbunge huyo wa Iramba Mashariki, ameapishwa leo Ijumaa Novemba 14, 2025 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Hatua ya kuapishwa kwake, inafungua rasmi milango ya kuanza utekelezaji wa majukumu ya mtendaji mkuu wa Serikali ya awamu ya sita kipindi cha pili.
Dk Mwigulu anashika nafasi hiyo kumrithi, Kassim Majaliwa aliyeongoza kwa miaka 10 tangu mwaka 2015.
Chanzo; Mwananchi