Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameungana na Watanzania kuomboleza kifo cha Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Kupitia ujumbe wake wa rambirambi, Dkt. Kikwete amemwelezea Kardinali Pengo kama kiongozi shupavu wa kiroho aliyetoa mchango mkubwa katika kuimarisha amani, umoja, na misingi ya maadili nchini Tanzania wakati wa uhai wake.
Dkt. Kikwete amekumbusha umuhimu wa utumishi uliotukuka wa Kardinali Pengo, akibainisha kuwa pengo lake litahisiwa si tu na waumini wa Kanisa Katoliki, bali na taifa zima kwa ujumla.
Ametoa pole kwa familia ya marehemu, Kanisa Katoliki, na Watanzania wote, huku akimuombea pumziko la amani kiongozi huyo aliyekuwa nguzo muhimu katika diplomasia ya kidini na ustawi wa jamii.
Chanzo; Itv