Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka Wakuu wa Wilaya wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia na kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha kuwapokea Wanafunzi mashuleni akisema Watoto walioripoti Shule hadi sasa ni 25% hivyo ameagiza msako wa nyumba kwa nyumba ufanyike ili Watoto warudi Shuleni.
RC Sendiga amesema hayo leo January 16,2026 banda ya kuona mahudhurio hafifu kwa wanaojiunga kidato cha kwanza Mkoani humo ambapo Mkoa ulitegemea kupokea Wanafunzi 28908 lakini hadi sasa waliohudhuria masomo ni asilimia 25 pekee.
Amewaasa Wazazi waliowaficha Watoto wao ili wasiende Shule kuacha mara moja tabia hiyo na mzazi atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Chanzo; Millard Ayo