Mbunge wa Kigoma mjini Clayton Chipando maarufu Baba Levo, amesema yeye atakuwa ni Mbunge wa tofauti katika kipindi chake cha uongozi akiwawakilisha Wananchi wa Kigoma na hatoweka mipaka kwa Wananchi akiwa mtaani ataishi maisha yao na akiwa ndani ya bunge atakuwa boss.
“Watu wengi wanasema Mbunge anabadilika anakuwa boss mimi nitakuwa tofauti kidogo kwasababu mimi nina amini watu ninaowaongoza wanataka niweje kwahiyo nikiwa bungeni nitakuwa kama boss nikiwa mtaani nitakuwa kama wananchi walionipigia kura” Baba Levo
Akizungumzia kuhusu post zake za kwenye mitandao ya kijamii amesema “komenti zitakuwa nyingi kwasababu mimi si Mtu maarufu na Watu wengi wanapiga ‘selfie’ bungeni ukigoogle picha za wanaopiga picha bungeni zinafika 4000 lakini ya kwangu inaleta taharuki kwasababu mimi ni Mtu maarufu” Clayton Chipando (Baba Levo) Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini.
Chanzo; Millard Ayo