Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema watendaji wa Serikali wasiobadilika kuendana na matarajio ya wananchi, atawabadilikia.
Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025, wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bunge la 13, ambapo pamoja na mambo mengine alitoa mwelekeo wa Serikali yake kwa miaka mitano ijayo.
“Watendaji msipobadilika kuendana na matarajio ya wananchi, tutawabadilikia. Nayasema haya mapema kwa watendaji walioko Serikalini na wale nitakaowateua kujitayarisha kisaikolojia na kujipanga vyema,” amesema Dkt. Samia.
Katika hotuba yake, Dkt. Samia amesema Watanzania wanahitaji mabadiliko chanya kwa maendeleo, hivyo watendaji wasipobadilika kuendana na mahitaji hayo atawabadilikia.
Chanzo; Global Publishers