Mahakama ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imewahukumu kifungo cha miaka ishirini jela Mashili Ndaki (48) Mayekra Kamwina (44) na Mayela Richard (38) wote wakazi wa Kaliua Mkoani Tabora baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na silaha mbili haramu aina ya gobore na vipande nane vya nyama ya kiboko.
Hukumu hiyo imetolewa Februari 11, 2026 na Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe. Fahamu Kibona.
Awali imeelezwa Mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo April 24, 2025 huko Sense ndani ya pori la akiba ugala.
Watuhumiwa hao walifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 23, 2025 na shauri hilo kusajiliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 8375 ya mwaka 2025
Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya mashahidi 5 ambapo mahakama hiyo imeeleza kuwa imeridhishwa na ushahidi uliotolewa pasi na shaka uliotosha kuwatia hatia watuhumiwa.
Chanzo; Bongo 5