Mwili wa Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, aliyekuwa Balozi wa Papa nchini New Zealand, unaagwa leo Alhamisi Septemba 25, 2025 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican.
Askofu Mkuu Rugambwa alifariki dunia Septemba 16, 2025 jijini Roma, Italia. Misa ya kumuombea na kuaga mwili wake imehudhuriwa na Watanzania wengi waishio Italia, kabla ya kusafirishwa kuletwa nchini kwa maziko.
Akizungumza na Mwananchi Septemba 21, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Jovitus Mwijage, alisema wanatarajia mwili huo utasafirishwa kesho Ijumaa, Septemba 26, kuletwa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ya Septemba 19, misa ya kumuaga itafanyika Jumamosi Septemba 27, 2025 saa 3:00 asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam.
Chanzo: Global Publishers