Wananchi kutoka kwenye kata za Utengule Usongwe, Nsalala na Bonde La Songwe Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi, halmashauri ya wialaya ya Mbeya wanalazimika kuamka saa tisa za usiku na kwenda ofisi za chama cha mapinduzi CCM tawi la Mbalizi ili kuwahi namba za kujiandikisha kupata vitambulishio wa taifa NIDA.
Zoezi hilo la usajili na utambuzi kwa wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya lilianza mwishoni mwa wiki iliyopita likiwa na matumaini makubwa kwa wananchi kupunguziwa adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa mkoa wa Mbeya lakini limekua na maumivu makali kwa wanachi hawa kuamka usiku na kupigana vikumbo ili kupata nafasi ya kujiandikisha.
Wasafi Media Tunapiga hodi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA mkoa wa Mbeya, tukitaka kujua ni jitihada zinachukuliwa na mamlaka ili kuwanusuru wananchi hawa na mazingira hatarishi nyakati za usiku wanapotoka nyumbani kwao hadi kituo cha kujiandikisha.
Chanzo; Wasafi Media