Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwinyi Awapa ACT Nafasi 4 za Uwaziri

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza Baraza jipya la Mawaziri ambalo litakuwa na jumla ya Wizara 20 ambapo amesema kuwa ameacha nafasi nne kwa ajili ya Chama cha Upinzani cha ACT-Wazalendo ambacho kitashirikiana kuunda Serikali ya umoja wa Kitaifa.

Dkt. Mwinyi ametangaza Baraza hilo jipya hii leo Novemba 13, 2025 katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Mnazi mmoja, Zanzibar ambapo amesema nafasi hizo nne za Mawaziri ni kwa ajili ya Chama chenye viti vingi vya Wawakilishi ambacho ni Chama cha ACT-Wazalendo na zimeachwa wazi kwa siku 90 kama Katiba ya Zanzibar inavyoeleza.

“Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar inataka Chama cha Upinzani ambacho kimepata Wajumbe wengi kwenye Baraza la Wawakilishi tuwapatie nafasi katika Baraza la Mawaziri na Chama pekee kilichopata Viti ni Chama cha ACT Wazalendo wamepata idadi ya viti 10 na kwa mujibu wa Katiba na fomula ya kupata Mawaziri wana nafasi nne za uwaziri, nimeamua kuziacha wazi bila uteuzi nafasi hizo mpaka pale tutakapokubaliana kama tutaingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa au laa kwa sababu niliahidi kushirikiana nao” - Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Aidha nafasi hizo nne zilizoachwa wazi ni pamoja na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ambayo ni sekta mama kwenye pato la Nchi, Wizara ya Biashara, Wizara ya Afya na Wizara ya Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais ambayo awali haikua kwa nafasi ya Chama hicho.

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: