Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ajiua kwa Kujikata Kolomeo

Gidion Mbwambo (34) mkazi wa eneo la Nguzo Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro, amekutwa akiwa amejiua kwa kujikata koromeo la shingo na kitu chenye makali katika.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama tukio hilo limetokea leo Januari 27 majira ya saa 11 alfajiri katika nyumba ya kulala wageni maarufu kwa jina la Kisanga iliyopo mtaa wa Nguzo Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Mkama anasema Mbwambo aligundulika amefariki dunia baada ya michirizi ya damu na maji kutokeza nje ya mlango wa chumba namba 106 alichokuwa amepanga.

Mkama anasema baada ya kuvunjwa kwa mlango uliofungwa kwa ndani ilibainika kuwa amefariki akiwa na jeraha la kujikata koromeo la shingo.

Anasema uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mbwambo amejiua kwa kutumia kitu chenye makali akiwa katika hali ya ulevi ambapo uchunguzi zaidi unaendelea.

Jeshi la polisi limewaagiza wamiliki wa nyumba za kulala wageni kufuata taratibu zote za kuwatambua wageni wanaolala katika nyumba hizo.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: