John Heche, Makama Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo “Chadema” ameongea kwa mara ya kwanza baada ya kuachiliwa kutoka mahabusu ambako amekaa kwa zaidi ya siku 20.
Wakiwa wameenda kuripoti polisi Novemba 11,2025 yeye pamoja na viongozi wengine wa Chadema ambao waliaachiwa hapo Novemba 10,2025 amesema hawajaachiwa kwa makubaliano yoyote.
“Kama tulivyokamatwa ndivyo tulivyoachiwa hakuna mazungumzo yoyote tuliyofanya na mtu yoyote nataka hili liwe wazi ili watu wasilete propaganda kwamba tumeachiliwa kwa makubaliano fulani.” - John Heche
“Bado sisi ni watu tunaamini ni innocent na tunataka watu wengine wote wanaoshikiriwa kinyume cha utaratibu waachiwe waende kwenye familia zao.”
Ikumbukwe Novemba 10,2025, John Heche, Godbless Lema, Boniface Jacob na Amani Golugwa waliachiwa kituo cha polisi kwa dhamana.
Chanzo: Tanzania Jornal