Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tulia Akikwepa Kinyang’anyiro cha Spika wa Bunge

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amejiondoa kwenye mbio za kutetea kiti hicho kwa awamu ya pili. Awali, Dk Tulia alichukua fomu za kuwania kutetea nafasi yake hiyo na kupitishwa na vikao vya uteuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini muda mfupi uliopita ametangaza kujiondoa kwenye mbio hizo.

CCM ilimpitisha Dk Tulia, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu na aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele.

Kujiondoa kwa Dk Tulia, ambaye pia ni mbunge mteule wa Uyole, kunamaanisha kwamba Zungu na Masele ndio wanabaki kuwania nafasi ya kuongoza mhimili huo.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: