Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabere, amesema jeshi hilo linaendelea kuwaandaa vijana kuwa mabalozi wa uzalendo wa kidijitali, watakaolinda heshima ya nchi katika mitandao ya kijamii na kukabiliana na watu wanaoichafua Tanzania mtandaoni.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa mujibu wa sheria katika kambi ya 822 KJ Rwamkoma, wilayani Butiama mkoani Mara, Meja Jenerali Mabere aliwataka vijana hao kuwa mstari wa mbele katika kuilinda nchi kwa nidhamu, heshima na uzalendo, sambamba na kuonesha mfano bora katika matumizi ya mitandao ya kijamii.
Kwa upande wao, vijana waliomaliza mafunzo hayo wameahidi kuwa mabalozi wema wa nchi katika mitandao ya kijamii, wakiahidi kutumia ujuzi walioupata kulinda amani, kuhamasisha maendeleo na kuimarisha umoja wa kitaifa.
Mafunzo hayo ya mujibu wa sheria yamehitimishwa Septemba 25, 2025 katika kambi ya 822 KJ Rwamkoma JKT, wilayani Butiama, mkoani Mara.
Chanzo: Wasafi