Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Matokea ya Uchaguzi Mkuu Kupingwa Zanzibar

Mahakama Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali maombi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika majimbo nane ya kisiwani Pemba, yaliyokuwa yamewasilishwa na wagombea kutoka Chama cha ACT-Wazalendo.

Jaji Haji Khamis Suleiman alitoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na pingamizi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, zilizobainisha kuwa maombi hayo yalikuwa na kasoro nyingi za kisheria ambazo zilizuia mahakama kuendelea na shauri hilo.

Sababu kuu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kasoro za kisheria zilizobainika kwenye hati za kiapo (affidavits) ambazo waombaji waliziwasilisha kama sehemu ya uthibitisho wao.

Mahakama ilijiridhisha kuwa kutokana na mapungufu hayo, hati hizo haziwezi kutambuliwa kisheria, jambo lililopelekea kufutwa kwa mashauri hayo ya majimbo ya Kiwani, Mkoani, Chake Chake, Chonga, Wawi, Wingwi, Micheweni, na Kojani.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: