Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mabasi ya Umeme Zanzibar Kuanza Kazi

Awamu ya kwanza ya mabasi yanayotumia umeme (ZanBus) yamewasili kupitia Bandari ya Malindi, Zanzibar.

Mabasi hayo 10, yamewasili jana Januari 25, 2026 katika Bandari ya Malindi na kuelekea katika maegesho ya stendi mpya ya Kijangwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zanzibar, leo Januari 26, 2026 imeeleza mabasi hayo yanatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi za usafiri wa abiria Februari 2026.

“Hatua hiyo inayolenga kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kuboresha usafiri rafiki kwa mazingira Zanzibar,” amesema.

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Raqey Mohamed amesema mradi huo, unaotarajiwa kuendelea kutekelezwa hatua kwa hatua, unaratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na utasimamiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Unitrans kutoka Afrika Kusini.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: