Mmoja ya viongozi waandamizi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania amekosoa kwa matamshi makali kile kilichotokea kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki katika wiki ya uchaguzi mkuu.
Jude Thaddaeus Ruwa'ichi ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam amesema Tanzania "imejeruhiwa" kutokana na vurumai iliyozuka wakati wa wiki ya uchaguzi.
Amesema simulizi zilizopo zinajumuisha "watu waliouawa kiholela wakiwa kwenye maandamano" ya kupinga uchaguzi na wengine waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi majumbani au maeneo mengine.
Akizungumza baada ya Misa Takatifu ya Kuombea Waliofariki wakati wa Uchaguzi Mkuu, Askofu Mkuu Ruwa´ichi amesema kilichotokea "ni kitendo kisicho na msamaha na ni chukizo mbele ya Mungu".
Hadi sasa serikali ya Tanzania hajiazungumzia chochote kuhusu madai ya mauaji ya kile upinzani unasema ni "maelfu ya watu" waliopigwa risasi na vikosi vya usalama walipoingia mitaani kupinga uchaguzi wa Oktoba 29.
Chanzo; Dw