Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Vijana Wanaochanganya Vinywaji Kutafuta Nguvu Zakiume Waonywa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Kitwana Idrisa Mustafa, amewaonya vijana wanaotumia vileo kwa kuvichanganya na vinywaji vingine, ikiwemo vya kuongeza nguvu (energy drinks), wakiamini kuwa huongeza nguvu za kiume.

Akizungumza leo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, huko Chukwani, Waziri Kitwana amesema imani hiyo haina uthibitisho wa kitaalam, hivyo inaweza kusababisha madhara makubwa kiafya.

Pia amekiri kuwapo kwa uingizwaji wa vileo vikali visiwani Zanzibar, akieleza kuwa bidhaa hiyo inaingizwa na baadhi ya wafanyabiashara wenye vibali halali.

"Changamoto kubwa haipo kwenye uingizwaji, bali ipo katika hatua ya usambazaji na uuzaji wake, ambapo baadhi ya wafanyabiashara huuza katika maeneo yasiyo rasmi kinyume na taratibu," amesema.

Waziri huyo amesema serikali imeanza kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti uuzaji wa vileo katika maduka ya kawaida mitaani, akisisitiza kuwa kitendo hicho ni kinyume na Sheria ya Udhibiti wa Vileo Zanzibar ya mwaka 2020.

Aidha, amewataka vijana kujiepusha na matumizi ya vileo vikali, kwa kuwa vina madhara makubwa kiafya na kijamii, ikiwemo kupunguza nguvu kazi ya taifa na kuathiri mustakabali wa vijana katika familia na jamii kwa ujumla.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: