Rais wa Urusi Vladimir Putin alimwambia Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Urusi itaupitia upya msimamo wake kuhusu mazungumzo ya amani baada ya kile ambacho Moscow imedai ni shambulio la droni la Ukraine kwenye makazi ya rais wa Urusi.
“Msimo wa Urusi Utabadilika baada ya shambulio la droni la Ukraine kwenye makazi ya Rais.” - Putin
Ukraine imepinga madai ya Urusi kwamba droni 91 zilishambulia makazi ya Putin kaskazini mwa Urusi, ikiyaita uongo, na imeishtaki Moscow kwa kujaribu kudhoofisha mazungumzo ya amani.
Mshauri wa sera za kigeni wa Kremlin, Yuri Ushakov, alisema kwamba Putin na Trump walizungumza Jumatatu na kwamba Putin alipewa taarifa na Trump pamoja na washauri wake wakuu kuhusu mazungumzo na Ukraine.
Putin alimjulisha Trump kuhusu shambulio la droni kwenye makazi ya rais wa Urusi na akamwambia Trump kwamba Urusi inapitia upya msimamo wake kutokana na tukio hilo.
Chanzo; Dw