Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Onyo!! Matumizi ya Barua Pepe Binafsi Serikalini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewataka watumishi wa umma kuacha kutumia barua pepe binafsi katika mawasiliano ya shughuli za Serikali.

Kikwete amesisitiza watumishi kutumia anuani rasmi za serikali na kusema matumizi ya barua pepe binafsi yamekuwa chanzo cha uvujaji na upotevu wa taarifa nyeti za serikali, hali inayohatarisha usalama wa taarifa hizo na kudhoofisha mifumo rasmi ya mawasiliano ya serikali.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Pili ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), amesema serikali imewekeza katika miundombinu ya TEHAMA inayokidhi viwango vya usalama na inapaswa kutumiwa ipasavyo na watumishi wote wa umma.

Amesisitiza kuwa kuanzia sasa serikali itafanya ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha taarifa za serikali zinawasilishwa kupitia barua pepe rasmi pekee, hatua itakayoongeza uwajibikaji na kulinda kumbukumbu za serikali kwa mujibu wa sheria.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Benedict Ndomba, amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za umma kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Barua Pepe Serikalini (GMS), ambao umetumika kwa zaidi ya miaka 10 na kuleta matokeo chanya katika mawasiliano na utekelezaji wa maamuzi.

 

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: