Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mkasa Mzima wa Kifo cha Mc Pilipili Wawekwa Wazi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kutokea kwa kifo cha Emmanuel Mathias Matebe maarufu kama MC Pilpili mkazi wa Swaswa Jijini Dodoma na Dar es Salaam, ambapo Novemba 16, 2025 majira saa 03:00 mchana marehemu alifariki katika kituo cha Afya Ilazo akiwa anapatiwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma Wiliam Mwanafupa amesema kuwa Kabla ya kufikishwa na umauti majira ya 02:00 mchana, msaidizi wa Mc Pilipili Hassan Ismail alipigiwa Simu na watu  asiowafahamu na kuomba wakutane na baada ya muda walifika watu watatu asiowafahamu wakiwa na Mc Pilipili ndani ya gari ndogo nyeupe na walimkabidhi Mc Pilipili akiwa na hali mbaya na wao kuondoka.

Kamanda Mwanafupa amendeleea kwa kueleza kuwa Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya umebaini, MC Pilpili alifariki dunia baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake na watu ambao bado hawajafahamika na kupelekea kifo chake.

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: