Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
Kupitia mtandao wake wa Instagram Rais Samia ameandika
"Ninawatakia nyote kheri katika maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kwa miaka 62 tumeendeleza dhamira ya msingi ya Mapinduzi ya kujenga jamii ya watu huru, yenye utu, yenye maendeleo, umoja, haki, amani na mshikamano"
"Sote tunao wajibu wa kuendelea kuzilinda tunu hizi na kuzirithisha kwa vizazi vijavyo, kama tulivyorithi toka kwa waasisi wetu".
Chanzo; Bongo 5