Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaonya Watu wanaoanzisha Kampuni na kuziita ni Kampuni za Wazawa wakati kiuhalisia zinamilikiwa na Wageni.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo hii leo Februari 16, 2026 akikagua mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara ya Kiserikali Mkoani humo.
“Wapo wasio waaminifu wanawatumia Watanzania kuanzisha Makampuni wanasema ni ya wazawa, tunataka kuinua Kampuni za Watanzania, upo mchezo Mgeni anatumia anuani ya Mtanzania ambaye si mnufaika, wale watakaogundulika wanafanya ujanja tutawafungia na hawatafanya kazi tena kwetu".
Chanzo; Millard Ayo