Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Dokta Ahukumiwa kwa Kuhujumu Uchumi, Matumizi Mabaya ya Mamlaka

Mnamo Febuari 10, 2026 mbele ya Mhe. Jasmin A. A wa Mahakama ya Wilaya ya Siha, TAKUKURU (W) Siha imefungua mashauri matatu ya Uhujumu Uchumi namba 2831, 2834 na 2837 ya mwaka 2026 ikiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Mshtakiwa Dkt. Donatus Boniphace Tsete ambaye ni Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Hospitali ya Taifa ya Kibong'oto iliyopo Wilaya ya Siha.

‎M‎shtakiwa huyo anakabiliwa na makosa saba kwenye kila shauri ambapo katika kosa la kwanza anashtakiwa kwa Matumizi Mabaya ya Mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/ 2007 ikisomwa pamoja na Aya ya 21, Jedwali la Kwanza, kifungu 57(1) na Kifungu cha 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Sura ya 200 marejeo ya Mwaka 2019, ambapo kwa kutumia cheo chake alifuja fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya usugu wa dawa za kifua kikuu (Drug- resistant Tubercolosis Mentorship) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same Shilingi 5, 082, 000, Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Shilingi 5,061,000 na Shilingi 5,490,000 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwenye kesi tatu.
‎Kosa la Pili likiwa ni Kughushi Kinyume na kifungu cha 333, 335(1) na 337 cha Kanuni za Adhabu sura ya 16 marejeo ya Mwaka 2022.

Aligushi saini kwenye attendance kuonesha kwamba washiriki wa mafunzo walisaini kulipwa fedha hizo.
‎Aidha, kosa la tatu likiwa ni kuandaa nyaraka zenye maelezo ya uongo kinyume na kifungu cha 342 na 337 cha Kanuni za Adhabu sura ya 16 marejeo ya Mwaka 2022. Nyaraka zenye maelezo ya uongo ni hati ya malipo na viambatisho vyake ambavyo ni dokezo sabili na pay list.

Kosa la nne ni kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 R.E 2019 hati ya malipo na viambatisho vyake ambavyo ni dokezo sabili, pay list.

Kosa la tano ni ubadhirifu wa fedha jumla ya Shilingi 15,633,000 kinyume na kifungu cha 28 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kosa la sita kuisababishia mamlaka hasara ya Shilingi 15,633,000 kinyume na Aya ya 21 ya jedwali la kwanza kifungu cha 57 (1) na 60 (2) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 toleo la 2

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: