Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Abdallah, Salehe Jela Miaka 30 kwa Unyang’anyi wa Kutumia Silaha

Mahakama ya Wilaya ya Kilindi, imewahukumu Abdallah Ally Lusewa (31), Salehe Mohamed Lusewa (23) na Salehe Shaban Mngoya (43), wakazi wa Kijiji cha Songe Wilaya ya Kilindi, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Tukio hilo lilitokea mnamo Juni 18, 2025 majira ya saa 04:47 usiku katika Kijiji cha Songe, ambapo mfanyabiashara Faraji Hamza Dole alivamiwa dukani kwake na kuibiwa mali mbalimbali zenye thamani ya shilingi 9,490,000/=.

Baada ya tukio kuripotiwa Polisi Songe – Kilindi, upelelezi ulianza mara moja na Julai 17, 2025 mtuhumiwa Abdallah Ally Lusewa alikamatwa na kuwatia mbaroni wenzake. Katika upekuzi uliofanywa nyumbani kwa Salehe Shaban Mngoya, zilipatikana televisheni mbili zilizoibiwa.

Baada ya upelelezi kukamilika, watuhumiwa walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kilindi chini ya kesi namba CC No. 19503/2025, na Februari 06, 2026, Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Bw. Toto Casmir iliwakuta na hatia na kuwahukumu kifungo cha miaka 30 jela.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: