Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Anayedai Kumuua Mwenyekiti CCM Aonywa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, limetoa taarifa likimuonya kijana mmoja anayejinasibu kumuua Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elia Richard Sambala, miaka 53, mkazi wa Itumbi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Taarifa ya polisi waliyoitoa kwenye ukurasa wao wa Instagram imesomeka hivi;

“Kupitia mitandao ya kijamii kunasambazwa picha mjongeo akionekana mtu mmoja mwanaume ambaye anajinasibu kuhusika katika tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Itumbi aitwaye Elia Richard Sambala, miaka 53, mkazi wa Itumbi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Ukweli ni kwamba, Februari 11, saa 7 mchana katika Kijiji cha Itumbi, Elia Richard Sambala, alikutwa shambani kwake akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye makali kichwani na watu wasiojulikana na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa matibabu.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, kupitia Askari wa kuchunguza matukio ya mauaji, walianza msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kuhusiana na tukio hilo na ufuatiliaji zaidi kwa wengine waliohusika unaendelea.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa masilahi wa eneo la uchimbaji madini ya dhahabu ambapo mmoja wa wanafamilia hao alikodisha kwa wawekezaji raia wa China kwa ajili ya shughuli za uchimbaji bila kushirikisha ndugu wengine.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa onyo kali kwa mtu huyo anayejinasibu kuwa ni kiongozi wa kikosi anachokiita TFF (Tanzania Freedom Fighters) kuacha kuongelea jambo ambalo ni tofauti na uhalisia na kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii kupotosha ukweli na kuhamasisha uhalifu dhidi ya Taasisi, Viongozi na Wananchi.

Upelelezi unaendelea na jitihada za kumtafuta mtu huyo ili kumkamata kwa hatua za kisheria zinaendelea.”

 

 

Chanzo; itv

Kuhusiana na mada hii: